Back to Swahili New Testament Bible online homepage (Contents Page of Online Bible)

 

Mark 15

[1] [2] [3] [4] [5] [6] [7] [8] [9] [10] [11] [12] [13] [14] [15] [16]

MK 15:1 Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
MK 15:2 Pilato akamwuliza Yesu, "Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?" Yesu akajibu, "Wewe umesema."
MK 15:3 Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi.
MK 15:4 Pilato akamwuliza tena Yesu, "Je, hujibu neno? Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juu yako."
MK 15:5 Lakini Yesu hakujibu neno, hata pilato akashangaa.
MK 15:6 Kila wakati wa sikukuu ya Pasaka, Pilato alikuwa na desturi ya kuwafungulia mfungwa mmoja waliyemtaka.
MK 15:7 Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
MK 15:8 Watu wengi wakamwendea Pilato wakamwomba awafanyie kama kawaida yake.
MK 15:9 Pilato akawauliza, "Je, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?"
MK 15:10 Alisema hivyo kwa sababu alijua wazi kwamba makuhani wakuu walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu ya wivu.
MK 15:11 Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba.
MK 15:12 Pilato akawauliza tena, "Basi, sasa mwataka nifanye nini na mtu huyu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?"
MK 15:13 Watu wote wakapaaza sauti tena: "Msulubishe!"
MK 15:14 Lakini Pilato akawauliza, "Kwa nini! Amefanya kosa gani?" Lakini wao wakazidi kupaaza sauti, "Msulubishe!"
MK 15:15 Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.
MK 15:16 Kisha askari walimpeleka Yesu ndani ukumbini, katika ikulu, wakakusanya kikosi kizima cha askari.
MK 15:17 Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamwekea kichwani.
MK 15:18 Wakaanza kumsalimu, "Shikamoo Mfalme wa Wayahudi!"
MK 15:19 Wakampiga kichwani kwa mwanzi, wakamtemea mate; wakampigia magoti na kumsujudia.
MK 15:20 Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
MK 15:21 Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba wa Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha auchukue msalaba wa Yesu.
MK 15:22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgotha, maana yake, "Mahali pa Fuvu la Kichwa."
MK 15:23 Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini yeye akaikataa.
MK 15:24 Basi, wakamsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura waamue nani angepata nini.
MK 15:25 Ilikuwa saa tatu asubuhi walipomsulubisha.
MK 15:26 Na mshtaka wake ulikuwa umeandikwa: "Mfalme wa Wayahudi."
MK 15:27 Pamoja naye waliwasulubisha wanyang`anyi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto.*fh* Matakatifu yanayosema, "Aliwekwa kundi moja na waovu."
MK 15:28 missing
MK 15:29 Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana, wakitikisa vichwa vyao na kusema, "Aha! Wewe mwenye kuvunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu!
MK 15:30 Sasa, shuka msalabani ujiokoe mwenyewe!"
MK 15:31 Nao makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria walimdhihaki wakisema, "Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
MK 15:32 Eti yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke msalabani ili tuone na kuamini." Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
MK 15:33 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa kulikuwa giza nchini kote.
MK 15:34 Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eloi, Eloi, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"
MK 15:35 Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hivyo, walisema, "Sikiliza! Anamwita Eliya!"
MK 15:36 Mtu mmoja akakimbia, akachovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, "Hebu tuone kama Eliya atakuja kumteremsha msalabani!"
MK 15:37 Yesu akapaaza sauti kubwa, akakata roho.
MK 15:38 Basi, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu mpaka chini.
MK 15:39 Jemadari mmoja aliyekuwa amesimama mbele yake aliona jinsi Yesu alivyolia kwa sauti na kukata roho, akasema, "Kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!"
MK 15:40 Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria toka mji wa Magdala, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
MK 15:41 Hawa walimfuata Yesu alipokuwa Galilaya na kumtumikia. Kulikuwa na wanawake wengine wengi waliokuja Yerusalemu pamoja naye.
MK 15:42 Wakati wa jioni ulikuwa umekwisha fika. Hiyo ilikuwa siku ya Maandalio, yaani siku inayotangulia Sabato.
MK 15:43 Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Armathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
MK 15:44 Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa. Basi, akamwita jemadari, akamwuliza kama Yesu alikuwa amekufa kitambo.
MK 15:45 Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu auchukue mwili wake.
MK 15:46 Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
MK 15:47 Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa.

 


Search the online bible

Back to Jesus Work Ministry main home page

Back to Jesus Work Ministry home for spiritual warfare and Christian deliverance ministry

Back to Jesus Work Ministry home for resources on Christian living

Christian deliverance and Spiritual warfare book 1

Christian deliverance and Spiritual warfare book 2

Christian deliverance and Spiritual warfare book 3

Christian deliverance and Spiritual warfare book 4

Spiritual warfare and Christian deliverance ministry classics

Other spiritual warfare and Christian deliverance resources on Jesus Work Ministry

Christian deliverance and spiritual warfare audio sermons (free Christian MP3 audio downloads)

Read online Bible - Swahili New Testament Bible online. Free online bible on SpiritualWarfare.JesusWork.org -An evangelical online ministry website of Jesus Work Ministry revealing biblical truth and recent errors on spiritual warfare and deliverance ministry principles. Wrong spiritual warfare is harmful when practiced. Avoid the snare of end-time false doctrine and its sad consequences. Free deliverance and spiritual warfare books, spiritual warfare sermons, spiritual warfare audio sermons (free Christian mp3 downloads) and other resources reveal what is bible based and false Christian spiritual warfare and Christian deliverance. Spiritual growth and Christian living resources on spiritual warfare and Christian deliverance ministry principles.

Essential resources for fellow evangelicals whether in Pentecostalism, charismatic movement, Baptist, Presbyterian, AG, AME, non-denominations, Christian fundamentalists, moderates and liberals. Non-evangelicals and non-Christians most welcome. The Truth that brings true freedom knows no boundaries. Learn to distinguish between biblical and non-scripture based spiritual warfare, spiritual warfare prayers, deliverance prayers and other areas of deliverance ministry (deliverence ministry) such as casting out demons, binding demons, dealing with territorial spirits, breaking generational curses, etc.

Plus learn the truth on our spiritual armor (spiritual armour), spiritual weapons of warfare, prayer and fasting, the sword of the spirit, pleading the blood of Jesus, spiritual battles, fighting spiritual warfare, familiar spirits, spiritual authority, demonic attacks, demonic possession cases, demonic influence, casting out demons, demonic deliverance, spiritual healing, healing the wounded spirit, biblical financial freedom etc. Solving the confusion on what is spiritual warfare, deliverance ministry and bringing healing to victims of false doctrine practiced by some “deliverance ministries.” Ultimately revealing Christ, and his truth that came to set captives free from deception, spiritual bondage, the curse of the law and so on. “If you hold to my teaching, you are really my disciples. Then you will know the truth, and the truth will set you free,” Jn 8:31-32. “So if the Son sets you free, you will be free indeed,” Jn 8:36.