Back to Swahili New Testament Bible online homepage (Contents Page of Online Bible)

 

Matthew 9

[1] [2] [3] [4] [5] [6] [7] [8] [9] [10] [11] [12] [13] [14] [15] [16] [17] [18] [19] [20] [21] [22] [23] [24] [25] [26] [27]

MT 9:1 Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa na kufika katika mji wake.
MT 9:2 Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, "Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako."
MT 9:3 Baadhi ya walimu wa Sheria wakaanza kufikiri, "Mtu huyu anamkufuru Mungu!"
MT 9:4 Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, "Kwa nini mnawaza mabaya mioyoni mwenu?
MT 9:5 Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, `Umesamehewa dhambi zako`, au kusema, `Simama, utembee`?
MT 9:6 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani." Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, "Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako."
MT 9:7 Huyo mtu aliyekuwa amepooza akainuka, akaenda nyumbani kwake.
MT 9:8 Watu wote katika ule umati walipoona hayo, walishangaa na kuogopa; wakamtukuza Mungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna hiyo.
MT 9:9 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Basi, Yesu akamwambia, "Nifuate." Naye Mathayo akainuka, akamfuata.
MT 9:10 Yesu alipokuwa nyumbani*fc* ameketi kula chakula, watoza ushuru wengi na wahalifu walikuja wakaketi pamoja naye na wanafunzi wake.
MT 9:11 Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi wake, "Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?"
MT 9:12 Yesu aliwasikia, akasema, "Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi.
MT 9:13 Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: `Nataka huruma, wala si dhabihu.` Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi."
MT 9:14 Kisha wanafunzi wa Yohane mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, "Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?"
MT 9:15 Yesu akawajibu, "Je, walioalikwa arusini wanaweza kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga.
MT 9:16 "Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka.
MT 9:17 Wala hakuna mtu awekaye divai mpya katika viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila divai mpya hutiwa katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama."
MT 9:18 Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, "Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali njoo umwekee mkono wako naye ataishi."
MT 9:19 Yesu akaondoka pamoja na wanafunzi wake, akamfuata.
MT 9:20 Mama mmoja, mgonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake.
MT 9:21 Alifanya hivyo kwani alifikiri moyoni: "Nikigusa tu vazi lake, nitapona."
MT 9:22 Basi, Yesu akageuka akamwona, akamwambia, "Binti, jipe moyo! Imani yako imekuponya." Mama huyo akapona saa ileile.
MT 9:23 Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga filimbi na umati wa watu wanaofanya matanga,
MT 9:24 akasema, "Ondokeni hapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu." Nao wakamcheka.
MT 9:25 Basi, umati wa watu ulipoondolewa, Yesu aliingia ndani, akamshika huyo msichana mkono, naye akasimama.
MT 9:26 Habari hiyo ikavuma sana katika nchi ile yote.
MT 9:27 Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, "Mwana wa Daudi, utuhurumie!"
MT 9:28 Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawili wakamwendea, naye akawauliza, "Je, mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo hilo?" Nao wakamjibu, "Naam, Mheshimiwa."
MT 9:29 Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, "Na iwe kwenu kama mnavyoamini."
MT 9:30 Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: "Msimwambie mtu yeyote jambo hili."
MT 9:31 Lakini wao wakaondoka, wakaeneza habari za Yesu katika nchi ile yote.
MT 9:32 Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo.
MT 9:33 Mara tu huyo pepo alipotolewa, mtu huyo aliyekuwa bubu akaanza kuongea tena. Watu wakashangaa na kusema, "Jambo kama hili halijapata kuonekana katika Israeli!"
MT 9:34 Lakini Mafarisayo wakawa wanasema, "Anawatoa pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo wabaya."
MT 9:35 Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna.
MT 9:36 Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji.
MT 9:37 Hapo akawaambia wanafunzi wake, "Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache.
MT 9:38 Kwa hivyo mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake."

 


Search the online bible

Back to Jesus Work Ministry main home page

Back to Jesus Work Ministry home for spiritual warfare and Christian deliverance ministry

Back to Jesus Work Ministry home for resources on Christian living

Christian deliverance and Spiritual warfare book 1

Christian deliverance and Spiritual warfare book 2

Christian deliverance and Spiritual warfare book 3

Christian deliverance and Spiritual warfare book 4

Spiritual warfare and Christian deliverance ministry classics

Other spiritual warfare and Christian deliverance resources on Jesus Work Ministry

Christian deliverance and spiritual warfare audio sermons (free Christian MP3 audio downloads)

Read online Bible - Swahili New Testament Bible online. Free online bible on SpiritualWarfare.JesusWork.org -An evangelical online ministry website of Jesus Work Ministry revealing biblical truth and recent errors on spiritual warfare and deliverance ministry principles. Wrong spiritual warfare is harmful when practiced. Avoid the snare of end-time false doctrine and its sad consequences. Free deliverance and spiritual warfare books, spiritual warfare sermons, spiritual warfare audio sermons (free Christian mp3 downloads) and other resources reveal what is bible based and false Christian spiritual warfare and Christian deliverance. Spiritual growth and Christian living resources on spiritual warfare and Christian deliverance ministry principles.

Essential resources for fellow evangelicals whether in Pentecostalism, charismatic movement, Baptist, Presbyterian, AG, AME, non-denominations, Christian fundamentalists, moderates and liberals. Non-evangelicals and non-Christians most welcome. The Truth that brings true freedom knows no boundaries. Learn to distinguish between biblical and non-scripture based spiritual warfare, spiritual warfare prayers, deliverance prayers and other areas of deliverance ministry (deliverence ministry) such as casting out demons, binding demons, dealing with territorial spirits, breaking generational curses, etc.

Plus learn the truth on our spiritual armor (spiritual armour), spiritual weapons of warfare, prayer and fasting, the sword of the spirit, pleading the blood of Jesus, spiritual battles, fighting spiritual warfare, familiar spirits, spiritual authority, demonic attacks, demonic possession cases, demonic influence, casting out demons, demonic deliverance, spiritual healing, healing the wounded spirit, biblical financial freedom etc. Solving the confusion on what is spiritual warfare, deliverance ministry and bringing healing to victims of false doctrine practiced by some “deliverance ministries.” Ultimately revealing Christ, and his truth that came to set captives free from deception, spiritual bondage, the curse of the law and so on. “If you hold to my teaching, you are really my disciples. Then you will know the truth, and the truth will set you free,” Jn 8:31-32. “So if the Son sets you free, you will be free indeed,” Jn 8:36.