Back to Swahili New Testament Bible online homepage (Contents Page of Online Bible)
1 Corinthians 10 [1]
[2]
[3]
[4]
[5]
[6]
[7]
[8]
[9]
[10]
[11]
[12]
[13]
[14]
[15]
[16]
1COR 10:1 Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote walikuwa chini ya ulinzi wa lile wingu, na kwamba wote walivuka salama ile bahari.
1COR 10:2 Wote walibatizwa katika umoja na Mose kwa lile wingu na ile bahari.
1COR 10:3 Wote walikula chakula kilekile cha kiroho,
1COR 10:4 wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe.
1COR 10:5 Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
1COR 10:6 Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani.
1COR 10:7 Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: "Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza."
1COR 10:8 Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu ishirini na tatu elfu.
1COR 10:9 Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.
1COR 10:10 Wala msinung`unike kama baadhi yao walivyonung`unika, wakaangamizwa na Mwangamizi!
1COR 10:11 Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi, ambao mwisho wa nyakati unatukabili.
1COR 10:12 Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke.
1COR 10:13 Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
1COR 10:14 Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu.
1COR 10:15 Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo.
1COR 10:16 Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo?
1COR 10:17 Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo.
1COR 10:18 Chukueni, kwa mfano, Wayahudi wenyewe: kwao, wenye kula vilivyotambikiwa madhabahuni waliungana na hiyo madhabahu.
1COR 10:19 Nataka kusema nini, basi? Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu ni kitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, ni kitu kweli zaidi ya sanamu?
1COR 10:20 Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe ninyi muwe na ushirika na pepo.
1COR 10:21 Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya pepo.
1COR 10:22 Au je, tunataka kumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhani tuna nguvu zaidi kuliko yeye?
1COR 10:23 Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga.
1COR 10:24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ila faida ya mwenzake.
1COR 10:25 Kuleni chochote kile kiuzwacho sokoni bila ya kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu;
1COR 10:26 maana Maandiko yasema: "Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana."
1COR 10:27 Kama mtu ambaye si muumini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu.
1COR 10:28 Lakini mtu akiwaambieni: "Chakula hiki kimetambikiwa sanamu," basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.
1COR 10:29 Nasema, "kwa ajili ya dhamiri," si dhamiri yenu, bali dhamiri yake huyo aliyewaambieni. Mtaniuliza: "Kwa nini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?
1COR 10:30 Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuru Mungu, kwa nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwa ajili yake nimemshukuru Mungu?"
1COR 10:31 Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
1COR 10:32 Msiwe kikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwa kanisa la Mungu.
1COR 10:33 Muwe kama mimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bila kutafuta faida yangu mwenyewe ila faida ya wote, wapate kuokolewa.
Search the online bible
Back to Jesus Work Ministry main home page
Back to Jesus Work Ministry home for spiritual warfare and Christian deliverance ministry
Back to Jesus Work Ministry home for resources on Christian living
Christian deliverance and Spiritual warfare book 1
Christian deliverance and Spiritual warfare book 2
Christian deliverance and Spiritual warfare book 3
Christian deliverance and Spiritual warfare book 4
Spiritual warfare and Christian deliverance ministry classics
Other spiritual warfare and Christian deliverance resources on Jesus Work Ministry
Christian deliverance and spiritual warfare audio sermons (free Christian MP3 audio downloads)